0754-213588 MKUU WA SHULE
JAMUHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS-TAMISEMI
SHULE YA SEKONDARI MADIBIRA,
S.L.P. 72,
RUJEWA.
MBARALI – MBEYA.
0754-213588
KUMB.NA.MSS/JI/K.5/19/1/10.
JINA LA MWANAFUNZI
…………………………………………….
ANUANI …………………………………
YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE KIDATO CHA TANO
MWAKA 2020
1. Ninayo furaha kukuarifu kuwa umechaguliwa kujiunga kidato cha tano, shule ya sekondari Madibira Mwaka 2020
2. MAHALI SHULE ILIPO
Shule ya sekondari Madibira iko WILAYA YA MBARALI- MKOA WA MBEYA. Kama unatokea Mbeya panda mabasi ya Mbeya- Rujewa (Pandia kutuo cha Nanenane-Uyole) pia basi la moja kwa moja yaani Mbeya-Madibira linapatikana stand ya NANENANE kila siku kabla ya saa 5 asubuhi. Ukiteremka Rujewa stendi utayakuta mabasi ya Rujewa – Madibira (kuanzia saa 3:00 Asubuhi mpaka saa 9:00 Jioni usafiri unapatikana) hivyo hivyo kwa wanaotoka Songea /Njombe waelekee barabara ya Mbeya na kuteremkia Igawa -Rujewa. Umbali kutoka Rujewa hadi Madibira ni Kilometa 80 kuelekea kaskazini. Kwa wanaotoka njia ya Iringa/Dodoma/Morogoro/Dar-es-salaam wateremkie Mafinga wilaya ya Mufindi – Iringa. Usafiri wa Mafinga – Madibira unapatikana kuanzia saa 4:00Asubuhi hadi saa 9.30 jioni.(Kinyanambo-njiapanda ya Madibira) Umbali toka Mafinga hadi Madibira ni takribani kilometa 68 kuelekea Magharibi
3. Nauli :Rujewa-Madibira=Tshs 5,000/. Mbeya-Madibira=9,000/=. Mafinga-Madibira=5,000/=
4. Hali ya hewa ya Madibira ni ya joto (bonde la ufa Usangu) wakati wa mchana na baridi wakati wa usiku.
5. Unatakiwa kufika shuleni tarehe ................2020 asubuhi au kabla. Masomo yataanza tarehe ................2020 asubuhi. Tafadhali fika shuleni ukiwa na vifaa na michango yote uliyoagizwa.
6. Uaminifu, utii, juhudi, maarifa na nidhamu safi kwa ujumla vitakuwezesha kufanikiwa katika taaluma na kujijengea tabia nzuri na mwenenendo mzuri.
KARIBU SANA MADIBIRA SEKONDARI.
1.0. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
SARE YA SHULE
(i) Mashati mawili (2) meupe ya mikono mifupi aina ya tetron
(ii) Suruali mbili nyeusi zenye marinda (celebration) mbili au tatu. Kwa ajili ya unifomu. Pia suruali moja ya kaki kwa ajili ya kushindia ziwe na turn up na isiwe ya kubana (modal)
(iii) Mkanda wa rangi nyeusi wa suruali wa ngozi usio na picha wala maandishi/mapambo
(iv) Viatu vya ngozi rangi nyeusi( vya kamba na visiwe vya mchongoko na vyenye visigino vifupi)
(v) Soksi pea mbili nyeusi
(vi) Godoro ft 2 ½ x 6 kwa mwanafunzi wa bweni
(vii) Mashuka mawili rangi ya pink na bluu bahari
(viii) Chandarua cha mbu
(ix) Blanketi moja
(x) Sweta mbili za kijani wakati wa baridi na T – shirt ya rangi ya njano yenye nembo ya shule inapatikana shuleni kwa tshs. 5000/= (elfu tano tu)
(xi) Kila mwanafunzi aje na mavazi ya michezo yaani nguo zitakazo msitiri wakati wa michezo bukta, t-shirt (Taifa Stars rangi ya bluu), raba, n.k
(xii) Ream ya karatasi 01 kwa mwaka (A4)
(xiii) Dissecting kit kwa wanafunzi waliochaguliwa kwa tahasusi /combination ya CBG
(xiv) Scientific calculators kwa waliopangiwa michepuo ya Sayansi
(xv) Vyombo vya chakula(sahani, bakuli,kijiko, na kikombe)
(xvi) Ndoo mbili (kubwa moja(20l) na ndogo moja)
(xvii) Kwanja 1, jembe 1, fagio ya ndani(brush) na nje(chelewa)pamoja na Panga
(xviii) Vitabu vya masomo ya tahasusi husika aliyopangiwa mwanafunzi
(xix) NAKALA YA HATI YA MATOKEO (RESULT SLIP) YA KIDATO CHA NNE
(xx) Fomu ya afya (Medical examination form )iliyojazwa na kuthibitishwa na daktari wa Hospitali ya Serikali.(imeambatanishwa mwishoni)
NB: Shule ina upungufu mkubwa wa vitabu,hivyo unashauliwa kama unaweza jinunulie vitabu kulingana na mchepuo uliopangiwa kwa kufuata orodha ya vitabu vilivyo pendekezwa katika ukurasa wa mwisho.
ADA NA MICHANGO YA SHULE
a. Ada ya Shule kwa mwaka ni Tshs 20,000/=kwa mwanafunzi wa kutwa, na Tshs70.000/= kwa mwanafunzi wa bweni.unaweza kulipa kiasi cha Tshs 10,000/= kwa mwanafunzi wa kutwa na Tshs 35,000/=kwa mwanafunzi wa bweni kwa muhula au kulipa ada yote kwa mara moja.Fedha za ADA zilipwe kwenye akaunti ya Shule Na;61101100004 NMB(MADIBIRA SECONDARY SCHOOL REVENUE ) Tafadhari andika jina la mwanafunzi kwenye PAY IN SLIP
b. Michango inayotakiwa kulipwa na kila mzazi ni;
i. Shilingi 15,000/= kwa ajili ya ukarabati wa samani
ii. Shilingi 6,000/= kwa ajili ya kitambukisho na picha
iii. Shilingi 20,000/= kwa ajili ya taaluma
iv. Shilingi 30,000/= kwa ajili ya kuwalipa wapishi, walinzi, na vibarua wengine
v. Shilingi 2,000/= kwa ajili ya nembo ya shule
vi. Shilingi 10,000/= kwa matumizi yafuatayo; huduma ya kwanza 5,000/= na bima ya afya (CHF) 5,000/=
vii. SHILINGI 20,000 kwa ajili ya mitihani ya kujipima (MOCK)
viii. Shilingi 5,000/= fedha ya Tahadhari (haitarejeshwa)
Michango hii isiyo ADA yote ya kifungu (b) ilipwe katika akaunti Na;61101200054
(MADIBIRA SECONDARY SCHOOL PROJECTS)
2.0. SHERIA NA KANUNI ZA SHULE
Shule hii inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Wizara ya Elimu na 25 ya mwaka 1978. Aidha inazingatia miongozo yote inayotolewa na wizara yenye dhamana ya Elimu nchini. Unatakiwa kuzingatia mambo ya msingi yafuatayo:-
(i) Heshima kwa viongozi, wazazi, wafanyakazi wote, wanafunzi wengine na jamii kwa ujumla ni jambo la lazima
(ii) Mahudhurio mazuri katika kila shughuli ndani na nje ya shule ni muhimu
(iii) Kutimiza/kutekeleza kwa makini maandalio ya jioni (preparations)
(iv) Kuwahi katika kila shughuli ndani na nje ya shule.
(v) Kufahamu maelekezo juu ya kuwepo ndani na nje ya mipaka hiyo wakati wote wa uanafunzi wako hapa shuleni
(vi) Kutunza usafi wa mwili na mazingira ya shule
(vii) Kuvaa sare ya shule wakati wote unapotakiwa
(viii) Kuzingatia ratiba ya shule wakati wote.
3.0. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE.
(i) Wizi
(ii) Kutohudhuria masomo kwa zaidi ya siku 90 bila taarifa/utoro
(iii) Kugoma au kuhamasisha mgomo
(iv) Kutoa lugha chafu kwa wanafunzi wenzake, walimu,walezi na jamii kwa ujumla
(v) Kupigana na wanafunzi wenzake,kumpiga mwalimu, au mtu yeyote yule
(vi) Kusuka nyele , wanafunzi wote wanatakiwa kuwa na nywele fupi wakati wote
(vii) Kufuga ndevu
(viii) Ulevi/unywaji wa pombe na matumizi ya madawa ya kulevya na uvutaji sigara
(ix) Uasherati ,uhusiano wa jinsi moja, kuoa au kuolewa
(x) Kushiriki matendo ya uhalifu, siasa, na matendo yeyote yanayovunja sheria za nchi
(xi) Kusababisha mimba au kumpa mimba msichana
(xii) Kutembelea majumba ya starehe na nyumba za kulala wageni
(xiii) Kumiliki,kukutwa au kutumia simu ya mkononi katika mazingira ya Shule
(xiv) Kudharau bendera ya Taifa
(xv) Kufanya jaribio lolote la kujiua, au kutishia kujiua kama kunywa sumu,nk
(xvi) Uhaibifu wa mali ya umma kwa makusudi.
FORM FOR MEDICAL EXAMINATION
MADIBIRA SECONDARY SCHOOL
P.O.BOX 72, RUJEWA-MBARALI
To be completed by medical officer.
Full name:........................…………………………………………………………
Age……………………………Years…………………………Sex………
Blood count (Red and White)……………………………………………
Stool examination………............................................................................
Urine analysis…………………………………………………….............
Syphilis test……………………………………………………………………
Eye test……………………………………………………………………....
T.B test………………………………………………………………….............
Ears……………………………………………………………..................
Chest………………………………………………………………………
Spleen………………………………………………………………………………
Abdomen…………………………………………………………………………
ADDITIONAL INFORMATION eg physical or chronically family
disease,etc…………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………
I certify that the above named student is fit to peruse studies
Signature……………………………………………………………………………
Designation…………………………………………………………………………
Section………………………………………………………………………………..
Date…………………………………………………………………………
NOTE: Medical officer at the time of examination the individual for any aliments you note.
PUPILS:
You must bring this complete form when you come to school, no student may enroll without certificate of physical fitness.
……………………
LAZARO A. MALAMBUGI
LAZARO A. MALAMBUGI
HEAD SCHOOL
0754-213588
MADIBIRA SECONDARY SCHOOL
FOMU YA TAARIFA BINAFSI ZA MWANAFUNZI
SEHEMU A(Ijazwe na Mwanafunzi)
JINA KAMILI(Kama kwenye result slip)..............................................................
Tarehe ya kuzaliwa......................Kabila...................Dini/Dhehebu.......................
COMB uliyochaguliwa...................Shule nitokayo...........................................
Mahali niishipo.................................Mkoa......................Wilaya.................
Anwani yako: S.L.P..............................................................................
SEHEMU B: TAARIFA ZA WAZAZI/WALEZI
Jina la Baba/Mlezi...............................................................kazi yake..............................
Jinala Mama/Mlezi...............................................................kazi yake...............................
Wazazi/walezi wanaishi (wapi)............................ .pamoja/wametengana.......................
Anwani ya mzazi/mlezi: S.L.P................................................SIMU...............................
SIMU..............................
Wakati wa likizo zote nitakuwa kwa(mtaje)......................................Wapi.......................
SIMU......................
Nathibitisha kuwa taarifa nilizotoa hapo juu ni za kweli na sahihi:
Sahihi ya Mwanafunzi...............................Tarehe.................................
KUKUBALI NAFASI(Ijazwe na mwanafunzi mwenyewe)
Mimi...............................................Nimesoma maagizo na taratibu za Shule na Wizara kwa makini, na kuzielewa na nipo tayari kuzifuata,Hivyo nakubali nafasi niliyopewa na nitafika Shuleni siku/tarehe husika kama zilivyopangwa
Sahihi:................................Tarehe...........................
KUTOSHIRIKI MGOMO /FUJO /MAKOSA YA JINAI
MIMI............................................UMRI...............JINSI(ME) KE
NAAHIDI Kwamba nitakuwa mwadilifu na mwaminifu, na kwamba sita shiriki wala kusababishakuchochea
Mgomo kwa namna yeyote ile, na nitatoa taarifa kwa utawala pale nitakapoona viashiria vya mgomo/fujo au uvunjifu wa amani Shuleni .
Aidha naahidi kwamba hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi yangu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kufukuzwa shule iwapo nitabainika kuwa nimeshiriki katika makosa yaliyoainishwa katika kifungu hiki
SAHIHI................JINA LA MLEZI/MZAZI................................SAHIHI............TAREHE...
SEHEMU B FOMU YA MZAZI KUKIRI /KUKUBALIANA NA SHERIA NA KANUNI ZA KUMLIPIAMWANAE ADA NA MICHANGO MINGINE
(IJAZWE NA MZAZI/MLEZI
MIMI....................................ambaye ni..............................wa mwanafunzi huyu(uhusiano)
Nimesoma kwa makini maelekezo pamoja na Sheria za Shule katika fomu ya kujiunga na nipo tayari ajiunge na Shule hii, Nina ahidi kumtolea ada,michango na mahitaji mengine ili aweze kupata Elimu yake vizuri katika Shule hii. Aidha nitasaidiana na walezi/walimu wa Shule katika kumlea kijana huyu katika maadili mema, na kuitika wito wa kufika Shuleni pale nitakapohitajika.
Aidha taarifa zote za maendeleo ya taaluma za kijana huyu itanifikia zikitumwa kwa ;
Jina(mzazi/mlezi)..................................................................S.L.P..................................
Anwani yangu ya kudumu ni...............................................SIMU....................
Sahihi.............................Tarehe.......................
Ndugu zangu wanaoweza kumtembelea mwanafunzi picha, na namba zao za simu zimeorodheshwa hapa chini:
1. ............................................simu........................................
2. ............................................simu.......................................
3. ............................................simu.......................................
4. ............................................simu.......................................
|
|
|
|
1 2 3 4
(I) MAANDALIO YA JIONI:
1. Kila mwanafunzi anatakiwa ahudhurie maandalio ya jioni siku zote za wiki
( jumatatu hadi Jumapili saa 1:30 hadi saa 4:00 Usiku.)
2. Ili kufanikisha maandalio ya jioni, kila mwalimu wa somo atakuwa anatoa kazi na kuhakikisha kuwa kazi hizo zimefanywa.
3. Walimu wa zamu watakuwa wanasimamia maandalio ya joini kikamilifu.
(II) KUWAHI:
Kila mwanafunzi anatakiwa
1. Kuthamini muda
2. Kuwahi katika shughuli za shule kama zilivyopangwa katika ratiba ya kila siku
3. Kufika shuleni kwa tarehe zilizopangwa
4. Siku ya kufungua shule, atokapo likizo mwanao anatakiwa kuripoti tarehe na muda aliopangiwa, iwapo atachelewa kufika tarehe na saa aliyopangiwa hatapokelewa. Mzazi/mlezi aliyeandikishwa shuleni atalazimika kuja na mwanae shuleni ili apokelewe.
(III) SARE YA SHULE
Kila mwanafunzi anatakiwa kuwa katika sare ya shule wakati wote wa:-
1. Masomo darasani
2. Kutoka nje ya shule kwa shughuli za kishule
3. Baraza la shule
4. Kwenda hospitalini
5. Kwenda maandamanoni
6. Kazi za mikono (vazi la kazi)
7. Michezo
8. Kwenda kanisani au msikitini
(IV) MIPAKA YA SHULE.
Kila mwanafunzi azingatie mipaka ya shule kama ifuatavyo:-
1. Kutoka nje ya mipaka ya shule bila kibali cha Mkuu wa shule
2. Kutotembelea sehemu zifuatazo isipokuwa kwa kibali maalum
(a) Chumba cha walimu (staffroom)
(b) Ofisi za shule
(c) Maabara
(d) Jikoni
(e) Nyumba za walimu na wafanyakazi wasio walimu.
........................................
LAZARO A. MALAMBUGI
MKUU WA SHULE
0754-213588
ORODHA YA BAADHI YA VITABU VILIVYOPENDEKEZWA
HISTORY
1.Major Events in African History-Mwijage
2. The Political Economy, Imperialism-by Nabudere
3.Africa Since 1800-4th Edition-by Roland Oliver
4. How Europe Underdeveloped Africa-W.Rodney
5. Europe from 1815-by Peacock
6. Major Issues in Africa History-ICD
|
GEOGRAPHY
1.General Geography in Diagrams-RB Bunnet
2.Regional Geography-Nyambari Nyangwine
3.Photography Interpretation and Elementary Surveying for Secondary Level New edition-Dura
4.Certificate Human and Economic Geography-Morgan and Leong Chang
|
KISWAHILI
USHAIRI
1.Kimbunga-G.Gora (Taasisi ya Uchunguzi Kiswahili-TUKI 1994
2. Chungu Tanu-T.A Mvungi (Tanzania Publishing House)
3. Mapenzi Bora-S.Robert (Mkuki na Nyota)2003
4. Fungate ya Uhuru-M.S Khatibu(Macmillan and Aidan)
RIWAYA
1.Vuta nikuvute-Shafi(Mkuki na Nyota)1999
2. Kufikirika-S.Robert(Mkuki na Nyota)2003
3. Mfadhili-Hussein Tuwa(Mathew B/W and Stationaries) 2007
4. Usiku Utakapokwisha-Mbunda Msokile(Macmillan and Aidan)2007
TAMTHILIYA
1.Morani-E.Mbogo (DUP)
2. Kivuli kinaishi –Said Mohamed (Oxford University Press)
3. Kwenye Ukino wa Thim-E.Hussein(University Press)
|
GENERAL STUDIES
1.General Studies(Communication Skills far A-level-M-Kadeghe
2. General Studies Notes (For A-Level V&VI)G. Mshiu and N. Nyangwine
|
ENGLISH LANGUAGE
1.A complete Course for Form V&VI-Michael Kadeghe
2. Teaching English as a Foreign Language-G-Broughton et.Al
3. A grammar of Contemporary English-Quirk, et.Al
4. Longman English Grammar-L.G Alexander
5.The real English Textbook For Advanced Level-By Michael Kadeghe
Advanced English Dictionary
NOVEL
1.The Beautiful One Are Not Yet Born-A.K Amah
2.A Man of the PeopleC/.Achebe
3. Divine Providence-Mkuki na Nyota
4.BlackMamba-EAEP
POETRY
1.Selected Poems-Institute of Education
2.The Wonderful Surgeon and Other poems-Mkuki na Nyota
|
CHEMISTRY
1.Ramsden Chemistry
2. Understanding Chemistry
3.S.Chandi’s Chemistry XI
4. S.Chandi’s Chemistry XII
5.Advanced Chemistry
Chemistry Review Paper I&2
|
BIOLOGY
1.Biological Science-DJ Taylor
2.Understanding Biology
3.S.Chandi’s BIOLOGY XI
4. S.Chandi’s BIOLOGY XII
4.Advanced Level Biology
5.Biology Review Paper 1&2
|
BASIC APPLIED MATHEMATICS
1.Basic Applied Mathematics F5
2. Basic Applied Mathematics F6
|